Vigezo na Masharti
Ilisasishwa Mwisho: Januari 2026
Mkataba wa Vigezo vya Huduma
Kwa kutumia au kuingia kwenye mfumo wa JamiiFund, unakubali kufungwa na Vigezo na Masharti haya. Tafadhali yasome kwa makini kabla ya kuanzisha kampeni au kutoa michango.
Aina ya Mfumo wa JamiiFund
Mfumo wa kiteknolojia unaounganisha wachangiaji na kampeni, sio taasisi ya kifedha.
Mtoa miundombinu inayowezesha michango salama ya mitandao ya simu na kadi.
Waandaaji wanawajibika kikamilifu kwa ukweli wa kampeni na matumizi ya fedha.
Wajibu wa Akaunti ya Mtumiaji
- Kutoa taarifa sahihi za kitambulisho na mawasiliano.
- Kulinda usalama wa namba za siri na akaunti yako.
- Watumiaji lazima wawe na umri wa kuanzia miaka 18.
Mwongozo na Maadili ya Kampeni
- Fedha zilizochangwa lazima zitumike tu kwa lengo lililowekwa.
- Maelezo ya kampeni yenye uwazi, ukweli na yasiyo na udanganyifu.
- Kufuata kikamilifu sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ada za Mfumo na Utoaji wa Fedha
Ada za Mfumo na Miamala
Ada ya Mfumo 5%
Inatakatwa kwenye michango ya kampeni iliyofanikiwa tu.
Makato ya kawaida ya mitandao ya simu (M-Pesa, Airtel, Tigo) yanatumika kulingana na mtandao.
Utoaji wa Fedha na Uhakiki
- Uhakiki wa lazima wa vitambulisho na akaunti za benki.
- Uzuiaji wa kiotomatiki wa miamala yenye shaka kwa usalama.
5. Mambo Yasiyoruhusiwa
- • Kampeni za udanganyifu au utapeli wa mchango.
- • Matumizi mabaya ya fedha au shughuli zisizokubalika kisheria.
- • Kuingilia au kudukua mfumo kinyume cha sheria.
6. Ukomo wa Uwajibikaji
- • Maelezo yasiyo sahihi kutoka kwa waandaaji wa kampeni.
- • Kampeni kushindwa kufikia lengo lake la kifedha.
- • Itilafu zisizotarajiwa za mifumo ya malipo ya mtandao wa simu.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Una maswali kuhusu vigezo au sheria?